Katika miaka zaidi ya 20 ya kufundisha Kiswahili kwa wageni, sija-kutana na andiko la hadithi nzuri kama hizi alizoandika mwandi-ihi Marc Eichen. Ufundi wake wa kutumia vitushi halisi, na kuvis-ana kwa maumbo mbalimbali ya lugha ni wa kipekee! Hadithi tatu hizi ni mchango mkubwa katika ufundishaji wa Kiswahili na fasihi kwa wenyeji na ugenini. Zitawasaidia pakubwa walimu pamoja na wanafunzi kufahamu uhondo wa lugha za Kiswahili na Kiingereza kupitia vipengele mbalimbali vya lugha aliyotumia mwandishi. Ndugu Suleiman Khalfan na Abdulrahman Ndegwa vilevile wametoa tafsiri ya haki, wakilenga kabisa alichodhamiria mwandishi wa hadithi zenyewe. - Dr. David Kyeu Coordinator and Continuing Lecturer Center for African Studies University of California, Berkeley Hadithi katika kitabu cha Upepo, Mchanga, Anga ni fupi, lakini zenye maana. Hadithi hizi zimejikita katika mandhari ya visiwa vya Zanzibar, Afrika Mashariki, taswira hizi za wazi zinamwalika msomaji kuandamana na wahusika wanaopitia changamoto za kibinafsi ndani ya eneo linalobadilika kwa kasi kutokana na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, utalii, na hata mabadiliko ya tabianchi. Kitabu hiki kita-wavutia wanafunzi wa Kiswahili na Afrika Mashariki kwa ujumla, na kwa upana zaidi, wale wanaotaka kuelewa mivutano ya kitamaduni na mabadiliko yanayohusiana na utandawazi. - Caitlyn Bolton, PhD Chuo cha Boston
Informations légales : prix de location à la page 0,3100€. Cette information est donnée uniquement à titre indicatif conformément à la législation en vigueur.
Extrait
UPEPO, MCHANGA, ANGA HADITHI TATU
UPEPO, MCHANGA, ANGA HADITHITATU M A R CE I C H E N
Imetafsiriwa kwa Kiswaili na Sani Suleiman Kalfan na Abdulraman Ndegwa
Hii ni tafsiri ya kitabu kinacoitwa Wind, Sand, Sky: hree Stories kilicoandikwa na Marc Eicen katika luga ya Kiingereza. Tafsiri ya Kiswaili imecapiswa kwa mara ya kwanza na:
Hii ni kazi ya kubuni. Majina, wausika, biasara, mandari na matukio yote yaliyotajwa ni matokeo ya kubuni kwa mtunzi tu. Kufanana kwa aina yoyote na mtu yeyote wa kweli, aliye ai au aliyekufa, matukio au mandari ya kweli ni kwa baati tu.
Haki zote zimeifadiwa. Hairuusiwi kunakili, kuifadi, kucapisa kwa njia ya kielektroniki au mekaniki, kutoa vivuli, kurekodi au kubadili seemu yoyote ya kitabu iki kwa njia, namna au mfumo wowote bila idini ya maandisi kutoka kwa mcapisaji Mkuki na Nyota Publisers Ltd.
Tembelea tovuti yetu www.mkukinanyota.com kujua zaidi kuusu vitabu vyetu na jinsi pa kuvipata. Vilevile utaweza kusoma abari na maojiano ya waandisi pamoja na taarifa za matukio yote yanayousu vitabu kwa ujumla. Unaweza pia kujiunga na jarida pepe letu ili uwe wa kwanza kupata taarifa za matoleo mapya zitakazotumwa moja kwa moja kwenye sanduku la barua pepe yako.
Vitabu vya Mkuki na Nyota vinasambazwa nje ya Afrika na African Books Collective.
www.africanbookscollective.com
Deborah, kwa ajili ya mapenzi yangu kwako Tuko pamoja milele.
6
Utangulizi
Kupuuzwa
Kusubiri
Kutoroka
Maswali ya Majadiliano
YALIYOMO
9
15
35
53
103
UTANGULIZI
Unaweza kutarajia na kupanga. Na unapaswa kupanga. UsisahauPringles katika safari, zawadi kwa ajili ya rafiki zako, kichapishi, shampuu ya RM. Lakini unapaswa kujua mipango yako itakupeleka ufukweni tu. Baadhi ya sehemu, itabidi ujitose kwenye mto. Utalazimika kuhisi mawimbi yanataka kukupeleka mahali. Na itabidi uogelee.
- KutokaTo Die and Live in Zanzibar, 25 Machi 2016
Tangu mwanzoni, kitabu cha hadithi kama hiki, kilichoandikwa na mgeni, kila mara huibua maswali kuhusu umilisi wa utamaduni. Nani ana haki ya kuandika kuhusu Zanzibar, Tanzania na Afrika? Nikiweka kando historia yangu mwenyewe katika Zanzibar, mawazo yangu ya sasa kuhusu swali hili yanafuata vidokezo vya Alexander 1 2 Chee na Andrew Wille. Ni itikadi isiyo sawa kusema kwamba waandishi wanaweza /hawawezi kuandika kuhusu tamaduni