Nyuma Ya Pazia
254 pages
Swahili (generic)

Découvre YouScribe en t'inscrivant gratuitement

Je m'inscris

Nyuma Ya Pazia , livre ebook

-

Découvre YouScribe en t'inscrivant gratuitement

Je m'inscris
Obtenez un accès à la bibliothèque pour le consulter en ligne
En savoir plus
254 pages
Swahili (generic)
Obtenez un accès à la bibliothèque pour le consulter en ligne
En savoir plus

Description

Nyuma Ya Pazia or Behind the Curtain is about corruption involving the president, and his ministers who rob the country of Mafuriko or Abracadabra. President in conjunction with his Premier brought fake foreign insecticide company; Richmen to invest in power generation in Mafuriko. Through logrolling Richmen lands a very lucrative tender used as a conduit of stealing millions from the Central Bank. Richmen is used to syphon billions of dollars from the treasury. When people get wind of this theft, force the government to crumble thereby rulers are punished by being jailed or other being sentenced to death. The book satirizes African kleptocratic regimes.

Sujets

Informations

Publié par
Date de parution 02 février 2015
Nombre de lectures 5
EAN13 9789956792801
Langue Swahili (generic)
Poids de l'ouvrage 2 Mo

Informations légales : prix de location à la page 0,0800€. Cette information est donnée uniquement à titre indicatif conformément à la législation en vigueur.

Extrait

vifo. Kitabu kinaupiga kijembe tawala Isadi barani Afrika.
Nyuma Ya Pazia
Nkwazi Nkuzi Mhango
NYUMA YA PAZIA
Nkwazi Nkuzi Mhango Langaa Research & Publishing CIG Mankon, Bamenda
Publisher:LangaaRPCIG Langaa Research & Publishing Common Initiative Group P.O. Box 902 Mankon Bamenda North West Region Cameroon Langaagrp@gmail.comwww.langaa-rpcig.net Distributed in and outside N. America by African Books Collective orders@africanbookscollective.com www.africanbookscollective.com
ISBN: 9956-792-18-7 ©Nkwazi Nkuzi Mhango 2015DISCLAIMER All views expressed in this publication are those of the author and do not necessarily reflect the views of Langaa RPCIG.
ShukraniDaima nitamshukuru Mungu aliyenipa buruhani ya kuniwezesha kufanya kazi hii adhimu. Pia nitamshukuru mke wangu Nesaa. Nasema tena kwa kisambaahongea mndee ne ja wana. Sina nilichowahi kukosa kwa kukuoa wewe bali kupata zaidi na zaidi faraja na ithibati ya maisha. Pia watoto wangu,Nthethe (Kanthethe), Ndidziwa (Ndiza) Nthelezi, Ng’ani, Nkuzi na Nkwazi Jr,. Kwani katika maisha yangu yote ya uandishi na upiganiaji haki za binadamu wao wamechangia kwa njia ya kunikosa hasa niliposafiri au kutaka kuwa peke yangu. Wakati naandika huwa mkali na mwenye kuhitaji upweke ili nifikiri. Wao kwa bahati nzuri waliishaizoea hali hii. Hivyo kwa dhati kabisa sina jinsi ya kuwashukuru kwa kuelewa maana ya kila nililolifanya na kuliwaza. Kwa namna ya pekee namshukuru Philo Ikonya aliyehariri mswada na kuwa tayari kuutafsiri ukiachia mbali kuniunganisha na Langaa. Shukrani zangu ziende kwa wote walionipa kila aina ya hamasa kutoa kazi hii. Mwisho nawashukuru wote watakaokisoma na kukifanyia kazi kitabu hiki. Nkwazi Mhango. th 249 4 Ave, S:E Altona MB, R0G OB3 Kanada. Baruapepe:nkwazigatsha@yahoo.com Wavuti:mpayukaji.blogspot.com Karibu mlioko mbele hata nyuma ya pazia tukutane iii
kwenye uwanja wa haki tujadili mstakabali wetu. Tujadili na kufundishana jinsi ya kuacha na maisha ya upanya na upunda tunayoishi. Kila la heri.
iv
1 Ufisadi kama kutu Jua Kali i majira ya saa nne asubuhi nchini Mafuriko. Jua ni vibarNaza vipana. kali kweli kweli. Ni kali hasa kwa wasio na nyumba zenye umeme, viyoyozi, feni hata viambaza na Nengoma alidamka mapema kwenda kupanga foleni ya maji kule bondeni kwenye kijito Mgombezi ambacho nacho maji yake si salama. Kwani kuna wakati hukujaa vinyesi, mizoga lembe lembe hata wakati mwingine rangi kutoka kiwanda cha magunia kilichojengwa katikati ya makazi ya watu kutokana na mwenye kiwanda kuiweka mfukoni serikali, nacho si haba. Huyachafua kweli kweli. Maisha ya watu maskini wa eneo hili nayo yameishachafuliwa sanjari na uchafuzi wa mazingira. Mumewe Zengeni hawezi kuridhika na mambo yanavyokwenda hata kidogo. Haridhiki na chochote kusema ukweli. Siyo kula yake wala vaa yake ukiachia mbali msatakabali wake kama mtu na taifa. Zengeni katika vyote, anaona amesalitiwa kiasi cha maisha kumpiga chenga. Hofu yake huongezeka hasa akiangalia wasomi kama yeye wanavyoteseka asijue wasiobahatika kusoma hali ikoje. Maisha yake ni ya kulazimika na kulazimisha. Nengoma bado ni kinda. Naye kama mumewe, ni mwalimu tena wa Lugha akibobea kwenye fasihi. Ni binti wa kiafrika aliyeumbika vilivyo kwa viwango vya mtu mwenye akili timamu siyo hawa Ma-miss vinyago wanaoitwa Warembo wa taifa wakati ukweli ni milembe ya kimaadili kwa taifa.
1
“Tangu lini urembo kwa mwafrika ukawa mifupa na mwendo wa kunyonda nyonda kama mgonjwa wa ukimwi?” Alizoea kuuliza Zengeni huku akijisifu kwa kujua kuchagua chema kilichofundwa kikafundika na kusoma na kuelimika. Nengoma ni mama aliyejaliwa umbile la mahaba lenye mvuto wa kipekee. Ni mweusi aliyekorea. Mama wa haja aliyekamilika kila idara huku akiwa amelelewa kwenye maadili mema na ya kizamani hata kama ana kisomo cha kisasa ambacho hakikumzuzua kiasi cha kuwa mtumwa wa usasa usio usasa bali ulimbukeni na ujuha hakuna mfano. Ni mama anayehifadhi maungo yake akitembea kwa staha na tahadhari asimchokoze mtu. Japo shida za maisha zimepiga na kumfifisha, si haba. Kila jicho limuengalo, lau huondoka na ridhiko hata mtikisiko hata kujisema kimoyo moyo, “Mama limeumbika.” Zengeni alizoea kumkodolea macho; hasa alipokuwa akitupa mtandio wake kwa mdongea wa Kimwambao. Rangi yake ni ya asili. Mwili wake hauijui mikorogo wala majaribosi kila aina yaingizwayo Mafuriko na kufurika masoko. Haijui Ambi wala Claire. Tatizo la maji linawakera sana wakazi wa Uswekeni. Kwani wao na wana mazingira walipiga kelele kabla ya kiwanda kujengwa hadi makoo yakawakauka na mwisho wake wakakubali kushindwa baada ya serikali yao kuonyesha kutokuwa na masikio kusikia kilio chao wala macho kuona uharibifu usio kifani iliokuwa ikiubariki. Wanajihisi kusalitiwa na serikali waliyoichagua wenyewe. Lakini wafanye nini katika nchi yenye wingi wa masahibu kila namna? Wafanye nini kwenye nchi ambayo Mungu wake ni pesa afanyae matajiri hata wawe majambazi, majizi hata machizi kuabudiwa? Kama ni tafsiri ya nchi basi nchi hii ni nchi ya mahepe kimaanawia.
2
Nengoma anampita Zengeni ambaye anamkata jicho na kutabasamu. Akiwa hana hili wala lile, Zengeni anafumwa na mkewe akimkata jicho. Nengoma anamuuliza mumewe. “Mbona umeduwaa unanishangaa nini? Jitahidi ukubaliane na ukweli dear.” Zengeni hajibu na Nengoma anaachana na swali lile asijue moyoni Zengeni anajisifu kwa kujua kuchagua. Ukiongezea na utondoti na kikuba ambavyo huwa havibanduki maungoni mwake, si haba. Mashallah! Nengoma anarudia kuuliza kinachomshangaza Zengeni asijue mwenzie ndiyo hivyo tena! Zengeni hajibu. Nengoma analiacha swali lake bila jibu na kuingia ndani na kutua ndoo yake huku akihema na kulalamika kuchoka. “Mume wangu, kama hali ikiendelea kuwa hivi, siyo siri, maisha ya hapa yatatushinda. Hawa wanasiasa waongo walituahidi pepo sasa wanatupa jehanam na jongomeo! Hawana lolote. Ni matapaeli hata kama wana madaraka wanayofuja.” Anajisemea baada ya kurudi kuungana na mmewe kiambazani baada ya kutua ndoo ya maji. Inaonekana umbali wa kupata maji na uchafu wa maji vimemchefua roho kiasi fulani. Zengeni anageuka taratibu kujibu swali la mkewe anayemjongelea akiwa anajifuta jasho. Anaonyesha kuchoka. Anasema. “Mama we, unataka maisha yatushinde mara ngapi? Tunajikongoja kwa matumaini tukitegemea angalau kesho inaweza kuleta neema lakini mwisho wa yote nadama zinaongezeka. Imefikia mahali jana inakuwa bora kuliko leo!” Anatikisa kichwa kwa masikitiko. Anajipanga vizuri kigodani na kuendelea “Ila ujue wazi kuwa kukata tamaa au kukubali kushindwa ni kujizika hai. Lazima tupambane kila uchao na inshallah Mwenyezi Mungu
3
anasikia. Tuzidi kupambana mambo yatabadilika hata kama ni baada ya muda mrefu. Mgaagaa na upwa.” Anamkazi macho mkewe aliyekuwa akimsikiliza kwa makini na kuendelea, “Tumshukuru Subhana kwani hapa si haba. Siyo kama kwa mama Mzaramizi aliyetutesa kwa sababu ya banda lake la urithi. Wanasiasa kwa kusema wasichotenda na kutenda wasichosema ni kama wamelaaniwa.” Anakohoa kidogo na kuendelea. “Umesikia kashfa ya kampuni la Richmen Development and Innovations?” “Bwanawe nchi hii imekuwa donda ndugu la kashfa. Juzi kulikuwa na kashfa ya wizi Benki kuu. Kabla haujafumka huu kulikuwa na wizi wizara ya madini na nishati. Pia kumbuka ule wizi baba lao ambapo Rais mstaafu aligundulika kuwa na biashara za siri na chafu nje ya nchi. Sasa hatujapumua wizi tena mwingine! Je hii Richmen nayo siyo yao hao hao wakubwa? Maana ukichunguza vizuri hakuna wizi ambao hauna mkono wao. Mwe! Jamani hawa watu watakuja kuuza roho zetu hata makaburi ya babu zetu! Mipesa yote hii ya nini au kichaa cha kuona manoti?” Nengoma anaamua kuangusha kilio chake baada ya kupewa taarifa za kuwapo kashfa nyingine.“Huoni walivyonenepeana na kunoneana kama nune kwa maghusubu huku tukifanyiwa magube?” Anaongezea Nengoma.“Mama wewe kwa kunga na misamiati na kufunga nyama sina hamu kabisa!” Zengeni alimtania Nengoma. Nengoma anaonekana kuchukia na kustushwa na kashfa hii jahara. Naye anatikisa kichwa chake huku akiamka kuondoka kuelekea ndani kutoa jiko nje lau likolee moto. Alimrai mumewe. “Unaonaje ukanipa muda kidogo niangalie jiko langu; nirudi tuuguze madonda haya ya kuibiwa na kuzikwa na wale tuliodhani ni wenzetu wakati siyo?”Nengoma anamalizia rai yake huku anatokomea ndani ili aende akatoe jiko lau aliwashie nje lipulizwe na upepo ili
4
mkaa ushike moto mapema atungike maji ya chai haraka. Zengeni najibu, “Leo maongezi na chai fahuwa.” Anasema huku akitikisa kichwa kama ishara ya kukubaliana na pendekezo la mkewe ambaye hasikii alichosema. Mara kitambo kidogo, Nengoma anatoka ndani na jiko la mkaa ambalo tayari keshalilisha. Kama ada, jicho la Zengeni halibanduki maungoni mwake. Zamu hii Nengoma hakuona jinsi alivyokatwa jicho la mahaba. Hata hivyo aliishazoea. Maana hana jinsi ya kulaumu bali kujivuna. Maana ni mumewe tena wa kujichagulia. “Mtu chake bwana.” Alizoea kusema Zengeni alipokuwa akifumwa akiiba maungo aamuapo kujibu kama siyo kupuuzia kama alivyofanya kitambo. Siku moja Nembogha alimtania kuwa angelimfungulia mashitaka kwa kumkonyezea na kumkodolea. Wacha Zengeni acheke. Alizoea kujitetea kuwa nani angeweza kuiba chake mwenyewe? Na isitoshe hizi ni sheria za kipuuzi toka wataraghani ambazo tumezipwakia toka kwa wakoloni wanaotaka kutuchonganisha ili wazidi kutudhoofisha na kututawala kirahisi.”Nengoma alizoea kujibu kwa kulinganisha na watawala wanavyojiibia wenyewe mali za nchi yao.
5
  • Univers Univers
  • Ebooks Ebooks
  • Livres audio Livres audio
  • Presse Presse
  • Podcasts Podcasts
  • BD BD
  • Documents Documents