Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya

-

Livres
290 pages
Lire un extrait
Obtenez un accès à la bibliothèque pour le consulter en ligne
En savoir plus

Description

Fifty Years of Kiswahili in Kenya is a collection of articles that were presented at an international Kiswahili conference organized by the National Kiswahili Association (CHAKITA) Kenya in 2013, which was held at the Catholic University of Eastern Africa (CUEA). A few articles are however from a similar conference held in 2012 at Kenyatta University. The book exemplifies the importance of the Kiswahili language in various sectors of society. Therefore, within this book you will find articles that focus on the teaching of the Kiswahili language; Kiswahili as a tool for national economic development; the contribution of Kiswahili to national cohesion and integration; Kiswahili research in language and literature; Kiswahili and portrayal of women; children�s literature in Kiswahili; and how Sheng affects Kiswahili. In short, the articles herein are a testimony of how Kiswahili has developed in the last fifty years in Kenya. This is a very important book for Kiswahili students and teachers. It is also an invaluable text for Kiswahili enthusiasts and all those who recognize its contribution to society.

Sujets

Informations

Publié par
Date de parution 08 mai 2014
Nombre de visites sur la page 8
EAN13 9789966028495
Langue Swahili (generic)

Informations légales : prix de location à la page  €. Cette information est donnée uniquement à titre indicatif conformément à la législation en vigueur.

Signaler un problème
utangamano wa kitaifa; utaIti wa Kiswahili katika lugha na fasihi; Kiswahili
ISBN9966-028-48-X
9 7 8 9 9 6 6 0 2 8 4 8 8
0 8
YA
MIAKA HAMSINI YA KISWAHILI NCHINI KENYA
WAHARIRI:| Leonard Chacha | Miriam OsoreInyani Simala
MIAKA HAMSINI YA KISWAHILI NCHINI KENYA
MIAKA HAMSINI YA KISWAHILI NCHINI KENYA
WAHARIRI: Inyani SimalaLeonard ChachaMiriam Osore
Kimechapishwa na:
Twaweza Communications Jumba la Twaweza, Barabara ya Parklands Mpesi Lane S.L.P. 66872 - 00800 Nairobi, Kenya Simu: +(254) 020 269 4409; 0729 427740 Barua pepe: info@twawezacommunications.org Wavuti: www.twawezacommunications.org
© Haki ya kunakili ni ya Twaweza Communications na CHAKITA-Kenya
Chapa ya kwanza 2014
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupiga chapa, kutafsiri bila idhini ya Twaweza Communications na CHAKITA-Kenya.
ISBN 978 9966 028 48 8
Kimeruwazwa na Catherine Bosire Jalada limesanifiwa na Kolbe Press
Kimepigwa chapa na Franciscan Kolbe Press S.L.P. 468-00217 Limuru, Kenya Baruapepe: press@ofmconvkenya.org
Yaliyomo
DIBAJI ............................................................................................................................ vii SHUKRANI .................................................................................................................... ix WAANDISHI WA MAKALA ......................................................................................... x UTANGULIZI .............................................................................................................. xiii SHAIRI ......................................................................................................................... xxii
SEHEMU 1: MIAKA HAMSINI YA LUGHA NCHINI KENYA Miaka Hamsini ya Ujenzi wa Taswira ya Mwanamke katika Ushairi wa Kiswahili Nchini Kenya ............................................................................. 3 Clara Momanyi
Miaka Hamsini ya Fasihi ya Watoto katika Kiswahili Nchini Kenya: Maendeleo na Changamoto ............................................................... 16 Pamela Y.M. Ngugi
Kwa Miaka Hamsini Sheng Imekitunza Kiswahili au Imekiua? ........................... 34 Peter Githinji
SEHEMU 2: UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI WA KISWAHILI Ufundishaji wa Kiswahili Ughaibuni: Maendeleo na Changamoto ...................... 53 Kiarie Njogu
Ufundishaji wa Kiswahili Sekondari: Nafasi na Changamoto za Vitabu vya Kiada ........................................................................................................... 71 Ombito Elizabeth Khalili na Mamai Margaret Nasambu
Ufundishaji wa Kiswahili katika Nchi za Kigeni: Mfano wa Chuo Kikuu cha Syracuse ............................................................................................ 80 Miriam Osore na Brenda Midika
Changamoto za Kujifunza Kirai Nomino cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi: Mchango wa Vitabu vya Kozi Vilivyoidhinishwa .................... 93 Leah Mwangi, Leonard Chacha Mwita na Jacktone O. Onyango
YALIYOMOv
SEHEMU 3: KISWAHILI KAMA NYENZO YA MAENDELEO YA UCHUMI WA TAIFA Kiswahili kama Lugha ya Mawasiliano katika Shughuli za Benki: Changamoto za Tafsiri ................................................................................................ 107 Jacktone O. Onyango
Nafasi ya Kiswahili katika Utekelezaji wa Rajua 2030: Tathmini ya Kipindi cha Awali 2008 – 2012 ............................................................. 113 Sheila Ali Ryanga
SEHEMU 4: KISWAHILI, UWIANO WA KITAIFA NA UTANGAMANO Dhima ya Methali za Kiswahili katika Kuelimisha Jamii Kuhusu Uwiano na Utangamano wa Kitaifa ......................................................................... 133 Joseph Nyehita Maitaria
Miziki ya Kiswahili kama Chombo cha Kuhimiza Uwajibikaji katika Jamii: Nyimbo za Mbaraka Mwaruka Mwinshehe ........................................................... 151 Henry Indindi
Methali za Kiswahili kama Chombo cha Kusuluhisha Migogoro ya Kijamii ........................................................................................................................... 163 Joseph Nyehita Maitaria
SEHEMU 5: UTAFITI WA KISWAHILI: LUGHA NA FASIHI Najivunia Kuwa Mkenya: Utosarufi, Mtindo au Mabadiliko ya Lugha? ........... 179 Leonard Chacha Mwita
Je, Sheng ni Lahaja ya Kiswahili? Nadharia ya Utambulisho wa Maana ........... 188 Ayub Mukhwana
Tathmini ya Tafsiri ya Pendekezo la Katiba ya Kenya 2010 .................................. 201 Grace Wanja na Miriam Osore
Tafsiri ya Majina ya Pekee – Uchunguzi Kifani wa Majina ya Nchi .................... 220 Leonard Chacha Mwita
Lugha –Ishara Nchini Kenya: Katiba na Mustakabali Wake Kisera .................... 242 Inyani K. Simala
UHAKIKI WA KITABU Siri Sirini: Mshairi na Mfungwa. Kitabu cha 1 ........................................................ 261 Ombito Elizabeth Khalili
vi miaka hamsini ya kiswahili nchini kenya
DIBAJI
Tangu taifa la Kenya kupata uhuru mnamo Disemba 12, 1963 kumekuwa na hatua nyingi zilizopigwa ili kuimarisha Kiswahili kama lugha ya utambulisho wa utaifa na kujenga hisia za uzalendo. Baadhi ya hatua hizo zinaonekana katika mfumo wa elimu ambapo Kiswahili hufundishwa na kutanihiwa shuleni na vyuoni. Kiswahili pia hutumiwa bungeni na katika biashara mbalimbali. Umilisi wa lugha hii miongoni mwa umma unatia moyo. Watu wengi wa makamo huongea Kiswahili kwa ufasaha kuliko ilivyokuwa siku za nyuma na mielekeo hasi kuhusu lugha yetu ya taifa inaendelea kupungua. Jambo la kutia moyo zaidi ni kwamba hivi majuzi, Katiba ya Kenya katika Ibara ya Saba imeipa lugha hii hadhi kubwa kama lugha ya taifa na rasmi. Hadhi hii inatoa fursa kwa umma kupata hudumu kupitia lugha ya taifa. Lakini inabidi sasa pawekwe mikakati madhubuti ya kutekeleza agizo hili la kikatiba. Watetezi wa Kiswahili, kwa ushirika na Wizara ya Michezo, Utamaduni na Sanaa, wako mbioni kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa Sera ya Lugha za Kenya. Uti wa sera hiyo ni fursa iliyopewa Kiswahili. Tunatumaini kwamba Wizara itakamilisha Sera ya Lugha na kuhimiza bunge ipitishe Sheria ya utekelezaji wa sera hiyo. Tungetaka kuona lugha ya Kiswahili ikitumika serikalini, bungeni, mahakamani na katika shughuli za kijamii. Hii ndiyo lugha inayoweza kujenga uwiano na utangamano wa kitaifa.
Ni kutokana na hisia hizi ambapo Chama cha Kiswahili cha Taifa (Kenya) kwa ushirika na Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki, walijumuika kwa furaha katika Kongamano la kuadhimisha miaka 50 ya Kiswahili Nchini Kenya. Katika Kongamano hilo, tulifikia maamuzi yaliyoonyesha namna tunavyoweza kuimarisha Kiswahili nchini Kenya na katika ukanda wa Afrika Mashariki. Penye nia pana njia. Tuna nia ya kuifanya lugha ya Kiswahili nyenzo ya maendeleo katika ukanda huu. Uundaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki uliidhinishwa na Baraza la Mawaziri mnamo 2007. Hata hivyo baadhi ya mataifa yalichelewa kutia saini itifaki ya Kamisheni. Jamhuri ya Tanzania ilitia saini mnamo Julai 19, 2010, Jamhuri ya Uganda mnamo Septemba 12, 2013 na Jamhuri ya
dibajivii
Burundi ziliafiki itifaki zote zilizokuwa zimetiwa saini. Kamisheni itakuwa na kikao chake Zanzibar na tunatarajia kwamba itaanza kufanya kazi mnamo Julai 2014.
Kitabu hiki ni mkusanyiko wa baadhi ya makala zilizowasilishwa katika kongamano la 2013. Wahariri wamejitahidi kuzipanga mada hizo ili kuendeleza mada za msingi zilizojadiliwa. Sina shaka kwamba kitabu hiki kitatoa ndaro kwa masuala mbalimbali na ufumbuzi wake.
Prof. Kimani Njogu, Ph.D. Mwenyekiti Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA) – Kenya Februari, 2014
viii miaka hamsini ya kiswahili nchini kenya
SHUKRANI
Kitabu hiki ni zao la makala zilizowasilishwa katika Kongamano la Kimataifa la Kiswahili – CHAKITA lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki Agosti 21 – 23, 2013. Upeo mkubwa wa ufanisi wa kongamano hilo, ikiwa ni pamoja na kuchapishwa kwa kitabu hiki, ulitokana na msaada kutoka kwa mashirika mbalimbali kama Longhorn Publishers, Goethe Institute, Catholic University of Eastern Africa, Nation Media Group, Oxford University Press, Twaweza communications na Jomo Kenyatta Foundation. Mbali na mashirika hayo, wanachama wa kamati andalizi, Kamati kuu ya CHAKITA na washiriki wote wa kongamano hilo wanahitaji kutolewa shukrani kwa juhudi zao na pia mchango wao wa hali na mali.
shukraniix