Shajara ya Mwana Mzizima 4
193 pages
Swahili (generic)

Découvre YouScribe en t'inscrivant gratuitement

Je m'inscris

Shajara ya Mwana Mzizima 4 , livre ebook

Découvre YouScribe en t'inscrivant gratuitement

Je m'inscris
Obtenez un accès à la bibliothèque pour le consulter en ligne
En savoir plus
193 pages
Swahili (generic)
Obtenez un accès à la bibliothèque pour le consulter en ligne
En savoir plus

Description

This is the fourth part in the series of the history of Dar es salaam. This book is about Kariakoo, the first area where Africans were allowed to live and stay. It traces the history of the area before independence and up till the 1970’s.
Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu vya kumbukumbu ya sehemu na watu mashuhuri katika jiji la Dar es Salaam. Kitabu hiki ni cha tatu ambacho kinachoonesha jiji la Dar es Salaam kwa jicho la mkazi mwenyeji. Historia hii muhimu kutambua tulipotoka na tunapokwenda tusije sahau tukapotea. Pia itakuwa kitabu cha kurejelewa kwa wasomi wa historia.

Sujets

Informations

Publié par
Date de parution 27 janvier 2024
Nombre de lectures 0
EAN13 9789912982857
Langue Swahili (generic)
Poids de l'ouvrage 2 Mo

Informations légales : prix de location à la page 0,4950€. Cette information est donnée uniquement à titre indicatif conformément à la législation en vigueur.

Extrait

Kariakoo ilee! Ya Zamani! Shajara ya Mwana Mzizima 4
Alhaji Abdallah Mohammed Tambaza
Readit Books Ltd. Dar es Salaam
Readit Books Ltd. S. L. P. 20986, Dar es Salaam www.readitbooks.co.tz
© Alhaji Abdallah Mohammed Tambaza, 2023 Jalada: Readit Books Ltd
eISBN 978 99129828 5 7Kitabu hiki ni sehemu ya makala zilizotolewa katika magazeti ya Raia Mwema.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kupiga chapa au kukitoa kitabu hiki kwa jinsi yoyote ile bila ya idhini ya Readit Books Ltd.
ii
iii
YALIYOMOKwenye Kitovu cha Kariakoo ............................................................................. 1 Huduma za Jamii Kariakoo ................................................................................11 Maisha katika Mtaa wa Msimbazi ..................................................................23 Maisha katika Mtaa wa Msimbazi II ..............................................................34 Poni na Kodi ya Kichwa ......................................................................................46 Wapigania Uhuru wa Kariakoo .......................................................................58 Wazalendo Wengine Kariakoo ........................................................................70 Kutoka Mwembetogwa, mashariki hadi Queensway.............................81 Kutoka Mwembetogwa, mashariki hadi Queensway II.........................93 Mto Msimbazi na Wanakariakoo ................................................................. 103 Umoja wa Wana wa Kariakoo ....................................................................... 112 New Street ............................................................................................................. 124 New Street II ......................................................................................................... 136 New Street III ....................................................................................................... 146 New Street IV........................................................................................................ 158 Masjid Mwinyikheri Akida.............................................................................. 168 Usafiri wa Baiskeli.............................................................................................. 178
iv
Sura ya KwanzaKwenye Kitovu cha Kariakoo ila unapopata nafasi ya kuzungumza na vijana kutaka kujua uelewa Kwao wa historia ya nchi yetu, ni lazima utabaini kwamba kuna ombwe katika yale machache wayajuayo. Hayo ni pamoja na masuala ya harakati za ukombozi wa nchi yetu na maeneo muhimu ya kihistoria ya taifa hili. Lakini kubwa linalojitokeza, ni kule kukosa kuwafahamu watu mashuhuri - ukimwacha Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume -waliotoa mchango mkubwa katika ukombozi wetu kutoka katika minyororo ya ukoloni wa Mwingereza.
Mathalan, mji wa Dar es Salaam, tokea enzi hizo ukiitwa Mzizima, umekuwa na historia yenye kusisimua kwelikweli. Haikupinda wala haina matege, kama hii ambayo hufundishwa mashuleni. Hiyo ni pamoja
na barabara zake zilivyokuwa; maeneo yaliyo muhimu kama Mwembetogwa; Hospitali ya Muhimbili ilianzaje; Kariakoo na Soko la Kariakoo ilikuwaje; Jumba la Madobi ni nini na lilikuwa wapi; Pombe Shop ni wapi na kwanini ilikuwapo wakati huo. Halikadhalika, ni taasisi gani muhimu hazikuwapo miaka hiyo; ambazo zilisababisha wananchi kupata shida; wakati nchi ikiwa chini ya himaya ya watawala madhalimu Wazungu. Wakoloni wa Kiingereza,
tofauti kabisa na inavyofahamika na vijana wa leo, walikuwa wabaguzi wa rangi. Waliitawala nchi hii katika misingi na sera ambazo zilikuwa na malengo ya kumdumaza mtu mweusi abakie ‘mjinga’ na ‘mpumbavu’ wakati wote.  1
Kariakoo tuijuayo leo, yenye maghorofa na mahoteli ya kifahari, 1 haikuwa hivi wakati wa utawala kandamizi wa Malkia Elizabeth chini
ya magavana wake wakali - wasokota masharubu - waliojaa chuki na ukatili kwa raia wanyonge wanaowatawala. ‘Majizungu’ yale, yaliwaita wazee wetu kila mara kwenye ofisi zao bomani, na kuwadhalilisha kwa kuwachapa viboko vya matakoni kwa makosa madogo. Fimbo ya henzirani yenye manundu yaumizayo ndiyo iliyokuwa ikitumika na kuweka makovu - Ah! Ah! Ah! Usikie hivyohivyo uchungu wa fimbo ya
henzirani! Hausemeki! Mtu mzima wa namna hiyo huwa hana hadhi, wala heshima tena miongoni mwa jamii anamoishi, pindi inapojulikana 2 3 kwamba ametoka kuchapwa bakora na DC au PC .
Katika suala la makazi, Wazungu ambao walijiona kama wenyewe na 4 wenyeji vile, waliishi eneo mashuhuri la Oysterbay (Waswahili walishindwa kulitamka neno hilo la kigeni wakiliita ‘Mastabee’ ). Kwa
vile waliokuwa wakiishi huko walikuwa ni ‘mabwana wakubwa’ wa daraja la kwanza - Wazungu watupu. Eneo hilo lilijengewa ‘shopping centre’ (eneo maalumu ya maduka) lilojulikana kama Morogoro Stores, likisheheni mahitaji yote muhimu ya ‘kibinadamu’ hapohapo mahala
1 Malkia wa Uingereza kuanzia June 1953 hadi _ 20222 District Commissionerau Mkuu wa Wilaya (DC) 3 Provincial Commissionerau Mkuu wa Mkoa (PC) 4  Eneo la Masaki Dar es Salaam kwa sasa
2
pamoja. Jina la Masaki lililopewaOysterbay, limetokana na jina la kijiji kilichopo wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani. Moja ya barabara mashuhuri kule ‘Mastabee’, baada ya kuwa tumejitawala, ikapewa jina la Masaki. Pia kuna Mtaa wa Chole na Ruvu yote ilikuwa njia ya kwenda huko Mtaa wa Masaki. Hivyo basi, kidogokidogo eneo lote la ‘Mastabee’, likaanza kupata jina jipya la Masaki na lile la asili likawa limepotelea mbali.
5 Neno ‘oyster’, limetokana na neno la Kiingreza la samaki wenye magamba magumu (shell fish), waitwao ‘chaza’. Chaza huvuliwa kwa wingi kwenye Ghuba ya Daraja la Selandar; mahala ambapo ‘majibaridi’ kutoka Mto Msimbazi, hukutana na ‘majichumvi’ ya Bahari ya Hindi. Bay’ ni ghuba.Oysterbay, lilikuwa ni eneo lilotengwa mahsusi kwa ajili ya kukaa mabwana wakubwa wanaotawala; ili waiishi wakipunga upepo mwanana wa baharini, pamoja na nyumba zenye kupendeza zilizopambwa kwa maua ya waridi ikiwamo na miti ya kivuli ya mikungu na mikaratusi.
Wakati Wazungu wakiishi huko; raia wa jamii ya Kihindi walipangiwa kukaa eneo la pili kwa ubora la Upanga; na Waafrika (raia daraja la mwisho) waliomiliki eneo hilo kwa karne nyingi nyuma, waliondolewa kwa nguvu na kupelekwa Kariakoo na Kisutu; ambako mtu unaweza
5  Kisayansi ni jamii ya mollusca
3
6 kupafananisha au kupaita ‘Soweto ’ ya Dar es Salaam wakati huo. Neno Kariakoo, linatokana na harakati za Wakoloni. ‘Carrier Corpsni neno la Kiingereza lenye maana ya msafara wa wabebaji wa vifaa vya askari wa majeshi wa kivita wa Jeshi la Kiingereza ‘Kings African Rifles’. Waswahili pia kwa kushindwa kutamka KAR waliwaita askari Kea. Si ajabu wala hoja kuwa Waswahili kushindwa kutamka maneno fulani ya Kiingereza vizuri. Hata Wazungu nao walikuwa wanashindwa kutamka maneno ya Kiswahili vizuri. Sehemu ambapo msafara ulikuwa ukiishia kwa mapumziko, mahala hapo iliwekwa kambi yake. Askari hao waliweka kambi hapo ilipo soko la Kariakoo kwa sasa. Askari hao walikuwa wakiletwa kutoka nchi mbalimbali zilizokuwa chini ya himaya ya Uingereza. Walikusanywa ili waje kutoa huduma muhimu vitani kama vile wapishi, wapagazi au wabeba mizigo ya askari wakiwa vitani - kwa 7 jina jengine wakiitwa ‘auxiliary force ’ katika vita baina Mwingereza na
Mjerumani. Vita ilipokwisha, Kariakoo ikawa ni soko na sehemu ya kibiashara kwa raia wa kiafrika peke yao, kukiwa - pamoja na mambo mengine - na
huduma za posta na vituo vya mabasi ya kuelekea kwenye sehemu za nje ya mji wa Dar es Salaam. Jirani na soko la Kariakoo, kwenye Barabara ya Mkunguni kulikuwa
6  Eneo la mji wa Johannesburg Afrika ya Kusini wanapoishi watu weusi katika kipindi cha ubaguzi wa rangi wa Makaburu 7  Kikosi kisichokuwa cha wapiganaji lakini wasaidizi wa askari wapiganaji
4
na eneo la Mnadani ambapo vitu mbalimbali - sio vyakula - vilikuwa vikinadiwa, ikiwamo na nguo chakavu pamoja na samani za nyumbani.
Jirani na eneo la Mnadani, kulikuwa na jengo refu lilonyooka mithili ya godauni, ambalo lilikuwa likiitwa Soko la Chai. Soko la Chai lilikuwapo hapo kwa ajili ya kuwapatia wananchi
wahitaji huduma ya chai asubuhi. Soko la Chai, lilikuwa na watu wanaouza chai na vitafunio (maandazi, vitumbua na mikate ya kumimina) pamoja na maharage, huku wateja wakiwa wamekaa kwenye mabenchi. Wauzaji wa chai hiyo walikuwa wengi huku vizimba vikiwa zaidi ya hamsini.
Pembezoni mwa Soko la Chai, kulikuwa na ‘Lingo la Kuni’. Hapo, pamoja na miti ya kujengea nyumba na makuti ya kuezekea nyumba, pia ziliuzwa kuni. Biashara hiyo ilikuwa ya mfanyabiashara wa kizalendo Juma Mzee na baadaye kurithiwa na mwanawe Saad Juma Mzee aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Klabu mashuhuri ya soka nchini 8 Sunderland Sports Club . Lingo la Kuni, lilikuwa ni eneo muhimu sana siku hizo. Hapo ndipo zilipokuwa zikipatikana zana zote za ujenzi wa nyumba za wananchi. Eneo lote la Kariakoo, lilikuwa na nyumba zilizojengwa kwa miti na kukandikwa udongo mwekundu wa mfinyanzi. Nyumba hizo takriban zote zilikuwa zimeezekwa makuti yatokanayo na majani ya mnazi.
8  Imebadilishwa na kuitwa Simba Sports Club mwaka 1971
5
  • Univers Univers
  • Ebooks Ebooks
  • Livres audio Livres audio
  • Presse Presse
  • Podcasts Podcasts
  • BD BD
  • Documents Documents